Timu ya soka ya Yanga jana imefanikiwa kushika uongozi wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuifunga timu ya Afrika Lyon ya jijini Dar es Salaam kwa magoli 3-1.
Mchezaji Idd Mbaga ndiye alikuwa shujaa kwa upande wa Yanga Baada ya kuifungia timu hiyo magoli mawili na goli lingine lilifungwa na mchezaji wa kimataifa toka nchini Zambia Davies Mwape.Kwa upande wa timu ya Afrika Lyon goli lao lilipatikana baada ya beki wa timu ya Yanga Chacha Marwa kujifunga.
No comments:
Post a Comment