Mfanyabiashara wa Marekani Stan Kroenke (wa kwanza kushoto) ameongeza hisa zake katika klabu ya Arsenal na kufikia asilimia 62.89, na pia kukubali kutaka kununua hisa zote zilizosalia za klabu hiyo. Hamu ya kununua hisa zote ilikuja baada ya kampuni ya Kroenke (KSE) kununua hisa za Danny Fiszman asilimia 16.1 na za Lady Nina Bracewell-Smith asilimia 15.9.
Makubaliano yamefikiwa pia na kununua mtaji wa hisa uliosalia, huku Arsenal ikikadiriwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 731.
Kroenke alinunua asilimia 9.9 za hisa za Arsenal kwa mara ya kwanza mwaka 2007.
"Tumefurahia nafasi hii na kujihusisha zaidi na kuonesha nia na Arsenal," amesema Kroenke mwenye umri wa miaka 63, ambaye kampuni yake pia inamiliki timu ya mpira wa kikapu ya Denver Nuggets inayocheza ligi ya NBA, na pia timu ya Colorado Avalance ya ligi ya NHL, na St Louis Rams ya ligi ya NFL, na Colorado Rapids inayocheza ligi kuu ya soka Marekani.
Hisa nyingi zilizosalia ambazo Kroenke huenda akazinunua zinamilikiwa na bilionea wa Urusi Alisher Usmanov.BBC
Libeneka la Malanyingi Matukuta Karibun kutembelea wajameni!! Ndani ya hii blog tunakuletea mambo mbalimbali ya michezo burudani na kijamii na masuala ya vivutio vya utalii hapa nchini!
Monday, April 11, 2011
MCHUNGAJI AMBILIKILE MWASAPILA APEWA SIMU NA AIRTEL HUKO LOLIONDO!
Mchungaji Ambikile Mwasapile akipokea zawadi ya simu ya mkononi toka kwa meneja biashara wa Airtel mkoani Arusha ndugu Paschal Bikomagu.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro ndugu Elias Wawa Lali akizindua mtambo wa mawasiliano wa Airtel katika kijiji cha Samunge,Loliondo.Pembeni ni wawakilishi wa Airtel mkoani Arusha na Diwani wa kata ya Samunge wakishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro ndugu Elias Wawa Lali akizindua mtambo wa mawasiliano wa Airtel katika kijiji cha Samunge,Loliondo.Pembeni ni wawakilishi wa Airtel mkoani Arusha na Diwani wa kata ya Samunge wakishuhudia tukio hilo.
LEO:TUPO HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI KARIBUNI...............!!
Hii ndo mbuga ya Taifa ya hifadhi ya Mikumi ni miongoni mwa vivutio vya Utalii hapa Tanzania.Barabara kuu ya Tanzania na Zambia/Malawi inakatiza katikati ya Mbuga hii.Hifadhi ya Mikumi ina wanyama na ndege wa kila aina pia kuna lodge na camp site nzuri ndan ya hifadhi.
KARIBUNI MIKUMI NATIONAL PARK!!!
YANGA BINGWA MPYA MPYA WA TANZANIA BARA 2010-2011.
Timu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam imefanikiwa kulirejesha kombe la ubingwa wa Tanzania Bara baada ya kuifunga Timu ya Toto Afrika ya Mwanza kwa magoli 3-0.Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa huo baada ya kuwazidi uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa mahasimu wao wa jadi kwa wastani wa goli 1,Simba nayo jana iliifunga timu iliyokwishatelemka daraja ya Maji Maji kwa kwa magoli 4-1.
HONGERA YANGAAAAAAAA!!
Subscribe to:
Posts (Atom)