Monday, April 11, 2011

TIMU YA ARSENAL YAUZWA KWA MMAREKANI.

Mfanyabiashara wa Marekani Stan Kroenke (wa kwanza kushoto) ameongeza hisa zake katika klabu ya Arsenal na kufikia asilimia 62.89, na pia kukubali kutaka kununua hisa zote zilizosalia za klabu hiyo.       Hamu ya kununua hisa zote ilikuja baada ya kampuni ya Kroenke (KSE) kununua hisa za Danny Fiszman asilimia 16.1 na za Lady Nina Bracewell-Smith asilimia 15.9.
Makubaliano yamefikiwa pia na kununua mtaji wa hisa uliosalia, huku Arsenal ikikadiriwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 731.
Kroenke alinunua asilimia 9.9 za hisa za Arsenal kwa mara ya kwanza mwaka 2007.
"Tumefurahia nafasi hii na kujihusisha zaidi na kuonesha nia na Arsenal," amesema Kroenke mwenye umri wa miaka 63, ambaye kampuni yake pia inamiliki timu ya mpira wa kikapu ya Denver Nuggets inayocheza ligi ya NBA, na pia timu ya Colorado Avalance ya ligi ya NHL, na St Louis Rams ya ligi ya NFL, na Colorado Rapids inayocheza ligi kuu ya soka Marekani.
Hisa nyingi zilizosalia ambazo Kroenke huenda akazinunua zinamilikiwa na bilionea wa Urusi Alisher Usmanov.BBC

No comments:

Post a Comment