Saturday, January 15, 2011

HIVI HALI YA KISIASA ILIYOPO MKOANI ARUSHA,KIONGOZI MKUBWA WA NCHI ANA KAULI GANI?

Hali ya kisiasa mkoani Arusha imezidi kuwa tete ambapo mwenyekiti wa CHADEMA taifa amesema chama hicho kitatoa tamko kuhusu hali iliyojitokeza mkoani hupo.
Lakini tumeona pamoja na hali hiyo kiasi cha waziri wa mambo ya nchi za nje aliitisha mkutano na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na kuwaeleza hali ya kisiasa iliyojitokeza pamojana mauaji ya watu wa tatu(3).
Je,kiongozi mkubwa wa nchi hii na mwenyekiti wa chama cha cha Mapinduzi(CCM) Mh;Jakaya Kikwete anakauli gani na tukio hilo pia na msimamo wa chama chake kuhusu mazungumzo ya muafaka wa kisiasa mkoani Arusha?