Monday, April 11, 2011

TIMU YA ARSENAL YAUZWA KWA MMAREKANI.

Mfanyabiashara wa Marekani Stan Kroenke (wa kwanza kushoto) ameongeza hisa zake katika klabu ya Arsenal na kufikia asilimia 62.89, na pia kukubali kutaka kununua hisa zote zilizosalia za klabu hiyo.       Hamu ya kununua hisa zote ilikuja baada ya kampuni ya Kroenke (KSE) kununua hisa za Danny Fiszman asilimia 16.1 na za Lady Nina Bracewell-Smith asilimia 15.9.
Makubaliano yamefikiwa pia na kununua mtaji wa hisa uliosalia, huku Arsenal ikikadiriwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 731.
Kroenke alinunua asilimia 9.9 za hisa za Arsenal kwa mara ya kwanza mwaka 2007.
"Tumefurahia nafasi hii na kujihusisha zaidi na kuonesha nia na Arsenal," amesema Kroenke mwenye umri wa miaka 63, ambaye kampuni yake pia inamiliki timu ya mpira wa kikapu ya Denver Nuggets inayocheza ligi ya NBA, na pia timu ya Colorado Avalance ya ligi ya NHL, na St Louis Rams ya ligi ya NFL, na Colorado Rapids inayocheza ligi kuu ya soka Marekani.
Hisa nyingi zilizosalia ambazo Kroenke huenda akazinunua zinamilikiwa na bilionea wa Urusi Alisher Usmanov.BBC

MCHUNGAJI AMBILIKILE MWASAPILA APEWA SIMU NA AIRTEL HUKO LOLIONDO!

 Mchungaji Ambikile Mwasapile akipokea zawadi ya simu ya mkononi toka kwa meneja biashara wa Airtel mkoani Arusha ndugu Paschal Bikomagu.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro ndugu Elias Wawa Lali akizindua mtambo wa mawasiliano wa Airtel katika kijiji cha Samunge,Loliondo.Pembeni ni wawakilishi wa Airtel mkoani Arusha na Diwani wa kata ya Samunge wakishuhudia tukio hilo.

LEO:TUPO HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI KARIBUNI...............!!










Hii ndo mbuga ya Taifa ya hifadhi ya Mikumi ni miongoni mwa vivutio vya Utalii hapa Tanzania.Barabara kuu ya Tanzania na Zambia/Malawi inakatiza katikati ya Mbuga hii.Hifadhi ya Mikumi ina wanyama na ndege wa kila aina pia kuna lodge na camp site nzuri ndan ya hifadhi.
KARIBUNI MIKUMI NATIONAL PARK!!!

YANGA BINGWA MPYA MPYA WA TANZANIA BARA 2010-2011.



Timu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam imefanikiwa kulirejesha kombe la ubingwa wa Tanzania Bara baada ya kuifunga Timu ya Toto Afrika ya Mwanza kwa magoli 3-0.Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa huo baada ya kuwazidi uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa mahasimu wao wa jadi kwa wastani wa goli 1,Simba nayo jana iliifunga timu iliyokwishatelemka daraja ya Maji Maji kwa kwa magoli 4-1.
HONGERA YANGAAAAAAAA!!

Saturday, April 9, 2011

TIMU YA U23 MANYARA STARS WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

                                       Baadhi ya wachezaji wa U23 wakishuka kwenye gari.
                               Wakishusha unga wa ngano
                                   Wakiingiza ndani
                            Pia na maji ya kunywa yalikuwepo
                            Mrisho Ngasa akiwa amembeba mmoja wa watoto wa kituo hiko
                             Kocha Jamhuri Kihwelo akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo.

Timu hiyo ilikabidhi msaada huo kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha UMRA kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam.Kocha wa timu hiyo alsema msaada huo ni kutaka baraka kwenye mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya timu ya Cameroon katika kuwania kufuzu kwenye michuano ya Olimpiki 2012

TASWIRA YETU JIJINI MBEYA.

 Shule ya msingi Azimio ni miongoni mwa shule kongwe jijini Mbeya
 Hii ni Mbeya Hotel
 Enzi za kituo cha daladala cha dox eneo la Mwanjelwa.
Jengo maarufu la Baby Shangazi jijini Mbeya

MKAKATI WA MAPINDUZI YA KIJANI KATIKA KILIMO KWANZA HAPA NCHINI.

 Viongozi wa Serikali wapo katika mstari wa mbele kusimamia zoezi la Kilimo Kwanza.Hapa Waziri Mkuu. Mh. Mizengo Pinda akipokea msaada wa Matrekta toka kwa balozi wa India hapa nchuni.
 Moja ya matrekta yaliyokabidiwa serikalini toka China.
 Jamii ya kimasai wakilima huko Kilosa kwenye maadhimisho ya Mapinduzi ya Kijani.
Shamba la mfano kuhusu Kilimo kwanza.

MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA MBEYA AHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM)

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa,Raisi Jakaya Kikwete akimkabidhi Kadi mpya ya Chama hicho ndugu.Sambwee Shitambala aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Mbeya.Ndugu Shitambala ambaye aligombania ubunge kwa awamu mbili kwa tiketi ya Chadema katika Jimbo la Mbeya Vijijini na kushindwa na Mbunge wa sasa Mh. Lackson Mwajali.
Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu za CCM mkoani Dodoma hapo jana!!

Friday, April 8, 2011

ZAO LA KAHAWA MKOANI MBEYA

 Hali ya hewa nzuri yenye ubaridi huko Mbeya vijijini kuna mashamba ya kahawa.
 Shamba la Kahawa huko Mbozi
 Kahawa ikiwa katika hali ya kuanza kuiva.
 Mkulima akikoboa(Pulping) kahawa ya matunda baada ya kuchuma.
 Wakiwa katika kusafisha kahawa na kuokota kahawa isiyokobolewa Mbeya vijijini.
 Wafanyakazi wakichambua kwa kuokota kahawa zisizofaa(Mbuni)
Kahawa ikiwa kwenye madaraja(Grade) yake tayari kwa uonjaji(Liquoring) katika kiwanda huko Mbozi.